Visit National Business Portal for more procedures

Ardhi na Majengo

Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, ardhi yote itaendelea kuwa mali ya umma na kubaki chini ya udhamini wa Rais kwa niaba ya wananchi wa Tanzania.

Sheria inatambua aina tatu za ardhi, ambazo ni. Ardhi ya Jumla, Ardhi ya Kijiji na Ardhi ya Hifadhi:

  • Ardhi ya Jumla ni ardhi iliyopimwa kwa kawaida iliyopo katika maeneo ya miji au yanayozunguka miji.
  • Ardhi ya kijiji eneo ya vijijini nchini Tanzania. Baadhi ya ardhi ya vijiji imepimwa lakini ardhi kubwa bado haijapimwa. Ardhi ya kijiji haiwezi kutumiwa kwa uwekezaji mpaka ihawilishwe kuwa ardhi ya jumla.
  • Ardhi ya Hifadhi inajumuisha hifadhi kwa ajili ya misitu, hifadhi za wanyama pori na viwanja vya burudani.

Kupata ardhi kwa ajili ya wawekezaji

Wawekezaji wa kigeni wanaweza kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania ambako anapewa ‘‘ Haki ya Matumizi’’ ya ardhi. Kuna njia mbili ambazo wawekezaji wanaweza kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji:

1) Kuomba kutwaa ardhi kutoka katika kijiji halafu anafuata hatua zote zinazotakiwa mpaka ardhi ihawilishwe kutoka katika ardhi ya kijiji na kuwa ardhi ya jumla na kukabidhiwa TIC ili kutayarisha Haki ya Matumizi ya ardhi kwa mwekezaji.

2) Kununua ardhi kutoka kwa mtu au kampuni; mara baada ya mnunuzi na muuzaji kukubaliana kuhusu bei, muuzaji anatakiwa kukabidhi Hati Miliki ya ardhi kwa Kamishina wa Ardhi ili atoe upya hati hiyo kwa jina la TIC ambaye mwishoni atatayarisha Haki ya Matumizi ya ardhi kwa mwekezaji.

 

Vibali vya Ujenzi
Construction permits are issued by the Municipal council in the municipality where the construction will take place.
menuPic1 menuPic2 menuPic3