Visit National Business Portal for more procedures

Kulipa Kodi

Mamlaka ya Mapato Tanzania ina jukumu la kukusanya kodi nyingi nchini Tanzania. Mamlaka za Serikali za Mitaa pia zina mamlaka ya kukusanya baadhi ya kodi na tozo. Kodi zinaweza kuwa za moja kwa moja au zisiwe za moja kwa moja. Kodi za moja kwa moja hasa zinahusu kodi ya mapato wakati kodi zisizo za moja kwa moja zinahusu biashara ya kimataifa na ya mlaji. Njia za malipo ya kodi ni kwa zuio, kulipa kwa awamu na makadirio. Kwa kawaida kila mtu anatakiwa kulipa kodi kwa awamu na kwa makadirio. Njia ya zuio ipo tu kwa wale wanaotakiwa kuzuia kodi ambao ni :

  • Waajiri wanaofanya malipo yatakayojumuishwa katika kukokotoa mapato yanayostahili kutozwa kodi ya mtumishi kutokana na ajira;
  • Watu wanaolipa mapato ya uwekezaji (k.m. wale wanaolipa gawio, riba, malipo ya maliasili, kodi au mrabaha);
  • Watu wanaolipa ada ya huduma na malipo ya mkataba. Hata hivyo kuna yasiofuata utaratibu huo. Usajili wa kodi hufanywa katika vituo vya kodi vya TRA karibu na eneo lako la biashara. Kodi pia zinalipwa kupitia benki;

➢ Usajili wa kodi hufanywa katika vituo vya kodi vya TRA karibu na eneo lako la biashara. Kodi pia zinalipwa kupitia benki. Bofya h apa kupata orodha ya ofisi za mkoa za TRA.

Kupata namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) expand_more expand_less
Kila mlipa kodi ni lazima ajisajili kwa ajili ya Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi kabla ya kuanza kufanya biashara nchini Tanzania.
TIN kwa ajili ya kila mtu
TIN kwa kampuni
See more
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) expand_more expand_less
Usajili kwa ajili ya VAT
Biashara zote zenye mapato ya mwaka yanayofikia shilingi milioni 100 na kuendelea ni lazima wajiandikishe kwa ajili ya kodi ya ongezeko la thamani- VAT. Ni lazima kisheria kwa walipa kodi kununua Mashine za Fedha za Elektroni (za stakabadhi) kabla ya kupata cheti cha VAT. Kampuni zinakusanya VAT kwa niaba ya TRA wakati zinapouza bidhaa au kutoa huduma. Kampuni zinatakiwa kuwasilisha mapato ya kila mwezi yanayoonesha jumla ya mauzo na ununuzi katika biashara zao.
Tamko na malipo ya VAT
Mapato yataingizwa siku ya mwisho ya kazi ya kila mwezi baada ya mwisho wa kipindi cha kutoa taarifa ya fedha kilichoelezwa.
See more
Lipa Kadri Unavyopata (PAYE)
Lipa kadri Unavyopata ni Kodi ya mtu inayokatwa na mwajiri kutoka katika mishahara ya kila mwezi ya wafanyakazi. Waajiri wanatakiwa kuwasilisha makato ya kila mwezi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. Aidha wanatakiwa wawasilishe taarifa za kodi za nusu mwaka (Tamko) kuonesha taarifa za makato katika kipindi cha miezi sita.
Kulipa kodi ya Mapato
Kulipa kodi ya Zuio

Makundi yafuatayo yanatakiwa kuzuia kodi:
- Watu wanaolipa mapato ya uwekezaji (k.m. wale wanaolipa gawio, riba, malipo ya maliasili, kodi au mrabaha).
- atu wanaolipa ada ya huduma na malipo. Hata hivyo kuna yasiofuata utaratibu huo.

Kwa orodha ya viwango vya kodi ya zuio bofya haps. Kwa waajiri wanaolipa PAYE (aina nyingine ya kodi ya zuio), bofya hapa

Kulipa kodi ya kampuni au shirika
Kodi ya kampuni au shirika inajumuisha kodi ya mapato, kwa kampuni au shirika lolote lililoanzishwa, lililoandikishwa au lililosajiliwa kwa mujibu wa sheria yoyote iliyosajiliwa nchini Tanzania au kwingine kokote na chama chochote kisichoandikishwa au kikundi chochote cha watu lakini haijumuishi ubia au udhamini.
Kampuni au shirika linaweza kuwa na mapato yanayotokana na biashara au mapato ya uwekezaji. Jumla ya mapato ya kampuni au shirika yanatozwa asilimia 30.
Kulipa ushuru wa stempu
MANQUE TEXTE SWAHILI
Kulipa kodi ya majengo
Kodi ya majengo inatozwa kwa kiwango sawa kwa majengo yaliyothaminiwa na manispaa au halmashauri za miji. Kiwango cha kodi kinachotozwa kinatumiwa kwa mujibu wa ukubwa, matumizi na mahali jingo lilipo.
menuPic1 menuPic2 menuPic3