Visit National Business Portal for more procedures

Kuanzisha biashara

Biashara za Tanzania zinaweza kusajiliwa kama jina la biashara, kampuni ya nchini au kampuni ya kigeni.

Wakala ya Usajili na Utoaji wa Leseni za Biashara (BRELA) ina wajibu wa usajili wa biashara nchini Tanzania. BRELA inatoa hati za kutimiza masharti kwa kampuni za kigeni, hati za uandikishaji kwa kampuni za nchini na vyeti vya usajili kwa ajili ya umiliki wa mtu mmoja.. Baada ya hapo makampuni ni lazima yasajili biashara zao  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), the Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ana kutegemea shughuli zao za biashara wajisajili pia na Wizara ya Biashara na Viwanda ("Jedwali A") au Manispaa ("  Jedwali B").

Kuanzisha kampuni ya nchini expand_more expand_less
Kampuni ya Jedwali A

Kampuni za Jedwali ‘A’ zinapata leseni za biashara zao kutoka Wizara ya Biashara na Viwanda. Bofya hapa kuona biashara yako inaangukia kundi gani.

Kampuni ya Jedwali B

Kampuni za Jedwali ‘B’ zinapata leseni za biashara zao kutoka Wizara ya Biashara na Viwanda. Bofya hapa kuona biashara yako inaangukia kundi gani.

Uanzishaji kampuni (kupitia Ofisi za TIC)

Wawekezaji wanaotaka kuomba vivutio na hawajaandikishwa wanaweza kuanzisha kampuni kupitia ofisi za TIC alimradi uwekezaji wa miradi yao una thamani ya angalau USD 500,000 kwa wageni na USD 100,000 kwa Watanzania.

Kusajili kampuni kwa njia ya mtandao (itaanza hivi karibuni)
See more
Kusajili kampuni ya kigeni expand_more expand_less

Kampuni ya kigeni ni kampuni iliyoandikishwa au kusajiliwa nje ya Tanzania. Inaweza kuanzisha biashara nchini Tanzania kwa kufungua tawi la kampuni hiyo.

Usajili kampuni ya kigeni (utaratibu wa kawaida)
Kusajili kampuni ya kigeni (kupitia Ofisi za TIC)
TIC inawawezesha wawekezaji wa kigeni kusajili matawi ya kampuni zao za kigeni nchini Tanzania.
See more
Kusajili jina la biashara
Kusajili jina la biashara ni njia rahisi zaidi ya kuanzisha na kuendesha biashara Tanzania . Pia ni utaratibu usio ghali na rahisi kabisa kuutekeleza. Nchini Tanzania watu mmoja mmoja (wamiliki pekee) au wabia (ubia) wanaotaka kusajili biashara zao kama biashara binafsi badala ya kuwa kampuni wanaingizwa katika kundi la Majina ya Biashara.
Register business name online expand_more expand_less
Register business name online
See more
Kuongeza muda wa leseni ya biashara expand_more expand_less
Wizara ya Biashara na Viwanda imetangaza kipindi cha kuongeza muda wa leseni ya biashara kwa mwaka kuanzia Julai 2013. Kwa hiyo leseni za biashara hazitolewi tena bure.Biashara zote nchini Tanzania zinatakiwa ziombe leseni za biashara za mwaka kwa kuwa Serikali imerejea utaratibu wa Sheria ya Utoaji Leseni ya mwaka 1972 iliyoweka ukomo wa leseni za biashara kwa vipindi maalum.
Biashara zote zenye leseni zilizotolewa kati ya Julai 2004 na Juni 2013 i lazima wafike kwenye mamlaka zinazotoa leseni zinazohusika waongeze muda wa leseni zao baada ya kulipa ada stahili. Uongezaji wa muda wa leseni ni lazima ufanywe kabla ya tarehe 31 Desemba 2013
Leseni za biashara za Jedwali A
Leseni za biashara za Jedwali B
See more
menuPic1 menuPic2